MENU
Junior Stars Wang'aa “CECAFA UNDER 18"
11/29/2023 16:06 in Sports

Vijana wa timu ya Kenya wasiozidi umri wa miaka 18 wamepata ushindi wa pili dhidi  ya Rwanda 1-0 kwenye mashindano yanayo endelea ya CECAFA kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 18, katika kaunti za Kisumu na Kakamega. 

Junior Stars walipata bao lao la kipekee kupitia mshambuliaji Aldrine Kibet katika dakika ya 37, Tyrone  Kariuki anayesifiwa na mashabiki wengi wa kandanda nchini kwa ubunifu wake katika safu ya kati ,alionyesha mchezo wa hali ya juu sana katika ngarambe hio.

Vijana wa Salim Babu wanao pigiwa upato kutwaa kombe hili, walimlaza Sudan kwenye mchezo wa ufunguzi , mabao 5-0

Mabao yalifungwa na Louise Ingavi,Tyrone Kariuki,Aldrine Kibet,Inghavi na Ellie Owande.Mashabiki wengi wanasema kuwa hii ndio  Harambee Stars ya siku za usoni.

Kwa sasa Kenya wamefuzu kwenye nusu fainali, huku wakiwa wamesalia na mechi moja licha ya kuongoza kundi A wakiwa na alama 6,huku wakifuatwa na Rwanda na alama 3,Somalia na Sudan wanashikilia nafasi za 3 na nne bila pointi yeyote.

 

Story By: Linet Kiunga.

COMMENTS
Comment sent successfully!